Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Abna, likinukuu Shirika la Habari la Anadolu, Mwanasheria Mkuu wa Istanbul alitoa hati ya kukamatwa kwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni.
Kulingana na ripoti hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Istanbul ametoa hati za kukamatwa kwa watuhumiwa 37, ikiwemo mhalifu wa kivita, Benjamin Netanyahu, kwa tuhuma za mauaji ya halaiki (genocide).
Kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Netanyahu nchini Uturuki kunakuja wakati Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilipotoa hati za kukamatwa dhidi ya Netanyahu na waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni mwaka jana.
Kutumia njaa kama silaha, mauaji, mateso, na vitendo vingine visivyo vya kibinadamu ni miongoni mwa uhalifu uliofanywa na Netanyahu na viongozi wengine wa utawala wa Kizayuni huko Gaza na Palestina.
Your Comment